Programu na huduma · 03

Uwezeshaji wa Vijana

Jamii Wezeshi Youth Skills and Empowerment Programme

Mpiga picha akirekodi tukio

Lengo

Kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa vitendo, kujiajiri na kutumia vipaji vyao kujenga vyanzo vya mapato.

Huduma zinazolengwa

  • Mafunzo ya upigaji picha na utengenezaji wa video
  • Mafunzo ya urembo, makeup na saluni
  • Mafunzo ya masoko ya kidijitali
  • Elimu ya kuanzisha biashara zinazotokana na ujuzi
  • Mafunzo ya kujitangaza kitaalamu na kutafuta wateja
  • Kuunganisha vijana na fursa za kazi na ushirikiano, pale zinapopatikana

Walengwa

  • Vijana wanaotafuta ujuzi wa kujiajiri
  • Vijana wasio na ajira
  • Vijana wenye vipaji vya ubunifu
  • Vijana wanaotaka kuanzisha biashara
  • Vijana wanaotaka kukuza shughuli zao za kitaaluma