Programu na huduma · 01

Uwezeshaji wa Wanawake na Vikoba

Jamii Wezeshi Women Empowerment Programme

Wanawake washiriki wa semina

Lengo

Kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia elimu ya fedha, usimamizi wa Vikoba na maendeleo ya biashara.

Huduma zinazolengwa

  • Mafunzo ya kuanzisha na kusimamia vikundi vya Vikoba
  • Elimu ya kuweka akiba na kupanga matumizi
  • Elimu kuhusu faida na hatari za mikopo
  • Mafunzo ya kukuza biashara ndogo
  • Elimu ya masoko na matumizi ya teknolojia katika biashara
  • Ushauri wa kutathmini uwezo wa kurejesha mkopo kabla ya kukopa

Walengwa

  • Wanawake wenye vikundi vya Vikoba/VICOBA
  • Wanawake wanaoendesha biashara ndogo
  • Wanawake wanaotaka kuanzisha biashara
  • Vikundi vya kijamii vinavyolenga kujikwamua kiuchumi